Breaking News: Watu 87 wafa kwa mafuriko, maelfu wakosa makazi China

0
454

Mafuriko makubwa yameyakumba maeneo ya kaskazini na ukanda wa kati wa China na kuua watu 87 na maelfu kupoteza makazi yao.

Maeneo ya majimbo ya Hebei and Henan ndiyo yameathirika zaidi na mafuriko hayo yaliyoambatana na kuporomoka kwa udongo.

Karibu nyumba 50,000 zimeanguka kwenye jimbo la Hebei, ambapo watu 72 wamepoteza maisha na wengine 18,000 nyumba zao zimeharibiwa vibaya kwenye jimbo la Henan.

Mamlaka ya China wameahidi kutoa msaada wa fedha kwa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko ambapo inasadikiwa mamilioni ya watu wataathiriwa na mafuriko hayo.

Viongozi wa jimbo la Hebei wamesema kuwa watu 25 wamefariki katika mji wa Xingtai pekee wakati huo huo watu 300,000 wamehamishwa kutoka katika jimbo hilo.

Jimbo la Henan limeshuhudia vifo vya watu 15 hadi sasa na watu 72,000 wamehamishwa.

Kutokana na mafuriko hayo umeme umekatika na kumekuwepo na matatizo makubwa ya mawasiliano.

Mamlaka ya hali ya hewa imetupiwa lawama na wananchi kwa kushindwa kuwatahadharisha mapema juu ya mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Inakadiriwa zaidi ya hekta milioni 1.5 za mazao zimeharibiwa vibaya hali inayoweza kupelekea kukosekana kwa mapato ya kiuchumi yanayozidi $3bn.

china1

LEAVE A REPLY