Watu 80 waokolewa na majeshi ya Nigeria

0
215
Rescued Chibok schoolgirl Amina Ali Darsha Nkeki is escorted by the military as she walks through a hospital in Maiduguri, Borno state, Nigeria in this handout received May 19, 2016. Nigeria Military/Handout via REUTERS ATTENTION EDITORS - THIS IMAGE WAS PROVIDED BY A THIRD PARTY. EDITORIAL USE ONLY. NO RESALES. NO ARCHIVE.

Jeshi la Nigeria limetangaza kuwau wapiganaji 42 wa kundi la Boko Haram na kuwaokoa watu 80 waliokuwa wameshikiiwa mateka na kundi hilo kwenye msako wa Jumanne kwenye kijiji kimoja kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Mpaka sasa jeshi la Nigeria limeshatangaza kuwakomboa zaidi ya watu 10,000 waliokuwa wanashikiliwa mateka na kundi hilo kwa kipindi cha miezi 7 ya mwaka huu.

Watu waiookolewa Jumanne ni kundi la watoto 42 na wanawake 38 ambao walipelekwa kwenye kituo cha afya cha kijeshi kwaajili ya kupatiwa huduma mbalimbali.

Rais wa Nigeria, Muhammad Buhari aliapa kulitokomeza kundi la Boko Harama wakati wa kampeni zake za uchaguzi kabla ya kupata ridhaa ya wananchi na kumuondoa madarakani mtangulizi wake, Goodluck Jonathan.

LEAVE A REPLY