Watu 110 wamefariki kutokana na njaa nchini Somalia

0
163

Zaidi ya watu mia moja na kumi wamefariki kutokana na visa vinavyo husiana na ukame na baa la njaa katika eneo la kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Ukame mbaya unaokumba Somalia unatishia maisha wa mamilioni ya watu nchini humo.

Siku ya Jumanne Rais Mohamed Abdullahi Farmajo, alitangaza ukame huo kuwa janga la kitaifa.

Umoja wa Mataifa una kadiria watu milioni tano nchini Somalia, wanahitaji msaada wa dharura na kuongeza kuwa taifa hilo ni moja kati ya mataifa manne, yaliyo katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa.

Karibu watu 260,000 walifariki kutokana na baa njaa iliyokumba Somalia kuanzia mwaka 2010 na 2012.

Pia njaa imetangazwa katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini, ambayo ndiyo ya kwanza kutangazwa tangu ile ya Somalia ya mwaka 2011.

LEAVE A REPLY