Watengenezaji wa TV za ‘Vizio’ wapigwa faini ya Bilioni 5 kwa ‘udukuzi’

0
167

Kampuni ya kutengeneza TV ya Vizio ya Marekani imekubali kulipa fidia ya $2.2m (TZS4.9bn) ili kumaliza tuhuma zakukusanya taarifa za mwenendo wa watazamaji wa Televisheni ambao wanatumia TV za Vizio.

Tume ya biashara ya Marekani ‘The US Federal Trade Commission’ imedai kuwa TV za kisasa za Vizio zimekuwa zikirekodi taarifa za chaneli zinazotazamwa kwenye luninga hizo na kutuma taarifa chenye chumba cha kuhifadhai taarifa cha kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa FTC, taarifa hizo huuzwa kwa watu wengine wakiwemo makampuni ya biashara.

Hata hivyo kampuni ya Vizio imejitetea na kudai taarifa hizo haziwezi kubainisha watu binafsi.

FTC imedai kuwa kampuni ya Vizio ilianza kukusanya taarifa hizo tangu mwaka 2014 na mwenenndo huo umeathiri zaid ya televisheni milioni 11.

Kampuni hiyo imeamriwa na FTC kuweka wazi kwa wateja wake aina ya taarifa inazochukua,a matumizi yake na athari zake kisha kupata ruhusa ya wateja wake ili kuchukua taarifa hizo.

Pia Vizio imeamriwa kufuta taarifa ambazo tayari imeshazikusanya.

LEAVE A REPLY