Watangazaji wa Citizen ya Kenya wapata ajali ya ndege

0
215

Watangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV za nchini Kenya, wamenusurika kufa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kuelekea Karbanet, kupata ajali katika eneo la Kibra jijini Nairobi.

Taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama wa Ndege za Polisi, Rodgers Mbithi zinaeleza kwamba ndege hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Wilson, ikiwa na wanahabari watatu waliokuwa wakielekea kwenye mkutano wa NASA, ndipo ajali hiyo ilipotokea.

Ndege hiyo, CESNA 206 ilikuwa imewabeba watangazaji wa Citizen TV ambao ni Sam Ogina, Cameraman Mauritius Oduor na Joseph Njane wa Radio Citizen.

Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini nchini humo kutokana  na majeraha ya ajali hiyo.

LEAVE A REPLY