Wastara kuelekea India Februari 4 kwa matibabu

0
176

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunga na kusema kuwa februari 4 anatarajia kuelekea nchini India kwa ajili ya matibabu ya mguu wake unaomsumbua.

Wastara amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu safari hiyo mjini Mumbai nchini India.

Pia Wastara amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tatizo linalomsumbua na kuweza kumpatia kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya matibabu ya mguu pamoja na mgongo.

Amesema kuwa katika safari hiyo ataongozana na nesi mmoja kutoka hospitali ya TMJ pamoja na mtu mmoja kutoka katika familia yake ambapo matibabu yake yatafanyika katika hospitali ya Saifee iliyopo Mumbai na kutarajia matibabu hayo kuchukua takribani wiki tatu na zaidi.

Aidha msanii huyo ameishukuru wizara inayosimamia Tansia ya filamu kwa kumfariji katika kipindi hiki kigumu anachopitia huku akimshukuru Waziri mwenye dhamana na tasnia ya filamu nchini, Bodi ya Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa la Taifa pamoja na watanzania wote kwa kuonyesha upendo wa dhati kwake.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Joyce Fissoo amesema kuwa serikali kupitia bodi ya filamu inashukuru kwa kupata taarifa kamili ya safari ya msanii Wastari Issa ilipofikia kwani bodi ya filamu inapenda kumuona Wastara akiwa katika afya nzuri na kurudi katika hali yake ili aweze kuungana na wanatasnia wenzake kuendeleza tasnia ya filamu nchini.

LEAVE A REPLY