Wastara awafungukia Bongo Movie

0
192

Mugizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amesema hatokuja kumladhimisha mtu yeyote katika tasnia ya ‘bongo movie’ kumsaidia pesa ya kujitibia mguu unaomsumbua.

Wastara ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa baadhi ya watu kutomuamini kwa kile kinachomsumbua huku wengine wakidiriki hata kujaribu kumwambia anatafuta kiki kupitia tatizo hilo linalomsumbua la mguu wake.

Hata hivyo Wastara amesema hawezi kubadilisha fikra za watu wanavyofikilia kwa kuwa hayo ndiyo maisha yao ya kutoamini jambo lolote lile.

Amesema kuwa “Na kama kuna wasanii ambao wanaamini mimi siumwi siwezi kumladhimisha hata siku moja na ambaye atasema hatokuja kumtembelea Wastara kwa sababu haumwi au hana shida pesa, mimi siwezi kumfanya aniamini kwamba sina pesa. Sitoweza kufanya hicho kitu kwa sababu maelezo ninayoyaeleza katika runinga ndiyo yaleyale hayotokuja kubadilika. Kwa hiyo ninachoongea hapa ni ukweli hautokuja kubadilika miaka yote hata nikifa”.

Pamoja na hayo Wastara aliendelea kwa kusema “wapo watu wa kweli wanaoamini na wengine wasioamini ambao huwezi kuwafanya waniamini. Watanzania wanaoniamini mimi wanatosha kwa sababu mwisho wa siku sitokuja kujizika mwenyewe au kuzikwa na wasanii pekee yake”.

LEAVE A REPLY