Wastara atamani kujiua kisa kuibiwa

0
90

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kuweka wazi kuwa amepitia kipindi kigumu sana kiasi ya kwamba alitaka kujiua baada ya kuibiwa kila kitu.

Wasata amefunguka hayo baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumbani kwake, Sinza-kwa Remmy jijini Dar es Salaam na kumuibia vifaa vyote vya ‘production’ pamoja na vitu vingine.

Wastara amekuwa akisumbuliwa na tatizo la mguu wake wa kulia kwa muda mrefu bado amekuwa akipambana kujikimu kimaisha kupitia filamu zake.

Wastara alifunguka juu ya majanga yaliyomkuta huku akisema kuwa, imefika wakati anatamani asiwepo duniani kutokana na kuandamwa na matatizo.

Wastara ameweka wazi kuwa ameshawashirisha polisi juu ya janga hilo na anaamini ulikuwa ni mpango wa ndani uliofanywa na watu wake wa karibu.

LEAVE A REPLY