Wastara akanusha kutoka kimapenzi na Alikiba

0
97

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa hajawahi kutokana kimapenzi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba kama taarifa zinavyosambazwa.

Kauli ya mwanamuziki huyo imekuja baada ya taarifa kusambaa kuwa muigizaji huyo amewahi kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo.

Wasta amesemakuwa mwanamuziki huyo hana mahusiano naye zaidi kufahamiana kwa kawaida tu lakini anashangaa kuhusishwa kutoka nae kimapenzi kitu ambacho si cha ukweli kabisa.

Pia Wastara amesema kuwa kwasasa hana ukaribu na wasanii hao kama zamani kutokana na Team Kiba kumtukana sana kipindi ambacho kijana mmoja anayesemekana kuwa wa karibu na familia ya Alikiba kukamatwa akiwa kwake.

Mwigizaji huyo pia amesisitiza kuwa familia ya Alikiba ni watu wake wa karibu sana lakini ushirikiano wa mitandaoni aliacha tangu yalipomkuta matatizo hayo.

Vile vile amesema kuwa Alikiba nampenda na kama familia yangu na itabaki hivyo maana siwezi tena kumpost mitandaoni kama nilivyokuwa nafanya zamani nikijisikia tu kwasasa ni ngumu kutokana na yaliyotokea.

LEAVE A REPLY