Wastara akanusha kusaidiwa na Diamond

0
60

Baada ya kusambaa taarifa kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz alimsaidia muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma kwa ajili ya matibabu nchini India muigizaji huyo amekanusha taarifa hizo.

Wastara amekanusha tetesi zinazosamba katika mitandao kuwa amekuwa akisaidiwa na Diamond Platinum kila mara anapokuwa anapatwa na matatizo hasa ya ugonjwa unaomsumbua.

Amesema kuwa pamoja na kwmaba mara nyingi amekuwa akiomba msaada sana kwa Diamond Platinumz lakini hakuna hata siku moja ambayo mwanadada huyo amepata jibu la maana kutoka  kwa Diamond.

Wiki iliyopita Diamond alitoa pesa nyingi kwa ajili ya vijana na kima mama  wa Tandale ikiwa kama sehemu ya kurudisha shukrani kwao.

Muigizaji huyo aliwahi kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu yake ya mguu yanayomsumbua kila mara ambapo baadhi ya wadau nchini wamekuwa wakimchangia kwa ajili ya matibabu hayo.

LEAVE A REPLY