Wastara afunguka sababu ya kuvunjika kwa ndoa yake

0
70

Muigizaji wa Bongo Fleva, Wastara Juma amefunguka sababu ya kuvunjika kwa ndoa yake na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Donge Zanzibar Sadifa Juma, ambapo amesema hakuingia kwenye ndoa hiyo kwa kupenda bali ni kuogopa kuzini.

Wastara amesema kuwa “Nimeolewa sio kwamba nilikuwa napenda ila mwisho wa siku mimi ni muislam na sitaki kuzini, hakuna atakayeniongelea vizuri labda marehemu Sajuki kama angekuwa hai ndio angeweza kunielezea Wastara ni mwanamke wa aina gani”

Pia amesema kuwa “Kabla sijaingia kwenye ndoa mume wangu alikuwa anani-treat vizuri, ananitumia kama laki tatu au mbili baada ya kuingia kwenye ndoa ilikuwa mtihani kweli”

Ameongeza kwa kusema kuwa “Kwanza ndoa ilikuwa inasitasita, nilikuwa nikiongea naye kidogo nasikia anasema basi nikupe talaka, na hilo neno nilianza kulisikia siku kumi baada ya kuolewa”.

LEAVE A REPLY