Wastara afunguka sababu ya kuolewa

0
138

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa amekuwa hachoki kuolewa kila siku kwa sababu kuna kitu amekuwa akitafuta katika ndoa zake.

Wastara amesema kuwa mara nyingia mekuwa akiamini kuwa anaweza kupata faraja ya moyo wake endapo ataolewa lakini mambo yanakuwa tofauti na vile yanavyotakiw akuwa na ndio maana amkuwa hachoki kufanya hivyo.

Wastara amesema kuwa pia anakuwa akiamini kuwa ipo siku anaweza kupata baba bora wa watoto wake hivyo anaamua kuolewa kwa sababu ya watito wanaohitaji malezi bora ya baba na mama.

Wastara ambae kwa sasa amejiingiza pia katika muziki na mambo ya kujitolea kwa ajili ya jamii amekuwa akiiingia katika ndoa lakini hazikai muda mrefu na kuachika mara zote.

Muigizaji huyo amekuwa katika mapenzi mara kwa mara na mara nyingine kuolewa lakini mambo yamekuwa hayakwendi vizuri hivyo kuachika katika ndoa zake.

LEAVE A REPLY