Wastara afunguka maisha yake baada ya kupata ajali

0
160

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kudai kuwa maisha yake yamebadilika tokea alipopata ajali kwa mara ya kwanza na kuvunjika mguu.

Wastara amebainisha hayo jana wakati alivyokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Taifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam muda mchache kabla ya kuanza safari yake ya kuelekea nchini India.

“Natamani kuwa na ‘Foundation’ yangu, kituo cha watoto yatima kwa sababu tokea nilipopata ajali maisha yangu yamekuwa yakusaidiwa tu asilimia kubwa japo ni msanii na nina jina lakini vitu vingi nimekuwa nikifanya kwa kusaidiwa kwa hiyo natamani siku moja nije nami kusaidia watu. ‘I wish’ na nina amini kwa nguvu ya Mungu itatokea tu”.

Pamoja na hayo, Wastara ameendelea kwa kusema “nina washukuru sana vyombo vya habari wote kwa moyo wa upendo walionesha kwa sababu bila ya wao hata mimi nisingekuwa Wastara. Napenda kuwaambia watanzania kwamba tuamini sana maneno anayosema mtu kuliko neno analosema mtu mwingine kwa hiyo naamini kuna wengine watakuja na matatizo tujaribu kuwaangalia nawao pia”.

Kwa upande mwingine, Wastara amesema hata akirudi kutokea katika matibabu yake hafikilii kuacha sanaa ya filamu kutokana anafanya kazi hivyo kutoka ndani ya moyo wake.

LEAVE A REPLY