Wastara afunguka kutendwa na wanaume

0
8

Muigizaji wa Bongo Movie, Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa wanaume wengin huwa wanamtenda wanapokuwa kwenye mahusiani.

 

Wastara amesema kuwa, wanaume wengi wanapenda kumuumiza kutokana na jinsi alivyo huku wengine wakiwa hawana hata chembe ya huruma na kumuogopa Mwenyenzi Mungu.

 

Wastara anasema kuwa, anaumia mno kwa sababu hakuna mwanaume ambaye alimpa mapenzi ya kweli bila kumuumiza zaidi ya marehemu Sajuki ambaye naye alikuwa mwigizaji wa Bongo Movies.

 

Wastara amesema kuwa, wanaume wengi walikuja kwake kama kumsanifu na kumuachia maumivu kwani hawakuwa na mapenzi ya dhati kama ilivyokuwa kwa Sajuki.

 

“Hakuna ambaye hajawahi kuniumiza tangu alipofariki dunia mpenzi wangu, mume wangu, rafiki yangu Sajuki.

 

“Wengine wote waliokuja baada ya Sajuki walikuwa wakiniumiza tu na kutumia ulemavu wangu kama fimbo ya kunichapia bila kujali maumivu yangu.

 

“Nikiri tu kwamba, hakuna mwanaume aliyenipenda na atakayemfikia Sajuki,” anasema Wastara kwa uchungu.

Mbali na Sajuki, Wastara ambaye hajasikika kwa muda mrefu sasa, amepitia katika maisha ya uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa.

 

Mwaka 2000 alifunga ndoa na mwanaume anayeitwa Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares.

Nyuma ya hapo, Wastara alizaa mtoto mmoja na Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.

 

Mwaka 2003, Wastara alifunga ndoa na Sajuki ambaye alifariki dunia mwaka 2013. Walibahatika kuzaa mtoto mmoja aitwaye Farheen.

LEAVE A REPLY