Washiriki wa Black Panther waweka historia tuzo za Oscar

0
63

Washirika wawili katika filamu ya Black Panther wameweka historia katika tuzo ya Oscar kwa kuibuka washindi wa kwanza weusi katika vitengo walivyoshinda.

Ruth Carter alijizolea tuzo ya mbunifu bora wa mavazi na Hannah Beachler alishinda tuzo ya ubunifu wa filamu kwa pamoja na mshindi mwingine Jay Hart.

“Lilitarajiwa kwa muda mrefu,” Carter amesema katika hotuba yake. “Huenda Marvel imeunda shujaa wa kwanza mtu mweusi lakini kwa kutumia mavazi ya ubunifu tulimgeuza kuwa mfalme wa Afrika.”

Mshindi mwenza wa Oscar Halle Berry ni mojawapo ya waliotangualia kumpa hongera, Filamu nyingine alizobuni Carter ni pamoja na Amistad, Malcolm X na Selma.

Wakati huo huo , Beachler – ambaye amewahi kushughulika katika filamu ya Moonlight, Creed n akibao cha Beyonce Lemonade – alitoa heshima kwa mkurugenzi wa filamu ya Black Panther Ryan Coogler.

“Nasimama thabiti kuliko nilivyokuwa jana,” amewaambia watu waliokusanyika katika tuzo hiyo.

“Nasimama hapa kwasababu ya mwanamume aliyenipa mtazamo tofuati wa maisha, aliyenipa mahala salama, aliye na subira na aliye na utu na undugu.

LEAVE A REPLY