Wasanii watakiwa kujitambua

0
211

Wasanii wa muziki na Movie nchini wamesisitizwa juu ya umuhimu wa kujijenga uwezo, kujithamini na kujitangaza iwapo wanataka kuiinua tasnia ya sanaa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harisson Mwakyembe, katika kongamano la kujadili tasnia ya  uigizaji ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Suma JKT jijini Dar es Salaam.

Kongamano hilo liliandaliwa na Bodi ya Filamu nchini wakishirikiana na Chama cha Waigizaji ambalo liliwajumuisha waigizaji, watayarishaji na wadau wengine kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujitambua, kujithamini na kujitangaza.

Miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza Dkt. Mwakyembe ni  pamoja na kwamba wasanii kadhaa waliokuwa wakidai haki na malipo kwa kazi mbalimbali walizofanya hapo awali, tayari wamelipwa, akiwemo mwigizaji marehemu  Steven kanumba.

“Nimefurahi  kwamba kwa sasa mambo yanakuwa mazuri kwa kuwa jamaa wa State Entertainment wamelipa hela za marehemu Kanumba na ameshakabidhiwa mama yake na wamekubaliana watatengeneza filamu ambayo itaelezea maisha ya Kanumba,”.

 

Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo walikuwa ni wasanii maarufu wakiwemo Wema Sepetu, thea, Davina Dino na wengine.

 

Wema ambaye amekuwa akikumbwa na dhoruba ya kufungiwa mara kwa mara kufanya sanaa kutokana na vitendo vya kwenda kinyume na tasnia hiyo na maadili ya kitaifa, alisema marafiki zake ndiyo waliomfikisha alipo sasa.

 

LEAVE A REPLY