Wasanii wa Hip Hop anaowakubali Joh Makini

0
25

Msanii wa Hip Hop Joh Makini amewataja wasanii Lord Eyes, G Nako na Fid Q kama ndiyo wasanii pekee ambao wapo katika kizazi chake cha marapa wakali Bongo huku akimtoa mdogo wake Nikki wa Pili kwa kusema ana era yake tofauti.

Joh Makini aliwataja wasanii wa Hip Hop ambao anawakubali hapa Bongo kutokana na mchango wao katika sekta ya muziki.

“Kwenye kizazi changu mimi kuna marapa wakali wengi tu kama Lord Eyes, Gnako na FidQ lakini Nikki wa Pili simuweki hapa, yeye ana ‘era’ yake pia”

Amesema kuwa “Mimi na Lord Eyes tumetoka mbali tangu mihangaiko ya Arusha hadi kuja Dar na kukaa pamoja, hali yake ambayo aliipitia wote ilituhuzunisha lakini na hatukuwa na chakufanya  ulikuwa wakati mgumu kwetu”.

Joh Makini, Lord Eyes, Nikki wa Pili na G Nako ni wasanii wa HipHop ambao kwa pamoja wanatokea kwenye kampuni ya Weusi.

LEAVE A REPLY