Wasanii wa Bongo Fleva wakosa tuzo za Afrimma

0
71

Wasanii wa Bongo Fleva, Alikiba, Diamond Platnumz na Harmonize wameshindwa kutamba kwenye tuzo za Afrimma zilizotolewa nchini Marekani baada ya kukosa tuzo hizo.

Wasanii wengine waliokosa tuzo hizo ni Nandy, Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz, Navy Kenzo pamoja na Jux ambao wote walikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kwa upande wa Afrika Mashariki waliotamba ni Khaligraph Jones kutoka Kenya ambaye ameshinda tuzo kwenye kipengele cha ‘Rap African Act’ na Eddy Kenzo na Ykee Benda  kutoka Uganda wakichukua tuzo ya ‘Best Male East Africa’ na ya Msanii chipukizi.

Yemi Alade, Wizkid na Mr. Flavour hao wameshinda tuzo moja moja kwenye utoaji wa tuzo uliofanyika usiku wa kumkia leo nchini Marekani.

Wengine waliokuwa wanaiwakilisha Tanzania ni DJ-D Ommy, Tudy Thomas na Moses Iyobo ambaye alikuwa anawania kipengele cha Mtumbuizaji bora wa Mwaka kwenye tuzo hizo.

LEAVE A REPLY