Wasafi radio kuruka hewani

0
139
Diamond

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz anatarajia kuanza kurusha matangazo ya Wasafi radio baada ya kukamilisha taratibu za radio hiyo.

Wasafi imekuwa ikifanya vizuri na hata kufanikiwa kufungua Tv yao wenyewe na sasa lebel hiyo inataka kufanya kitu kingine kikubwa cha kuwasha Wasafi radio kwa ajili ya mashabiki wao na kukuza muziki wa Tanzania.

Lengo la wasafi ni kutaka kupunguza wimbi la vijana wanaolalamika kila siku kuwa wamekuwa wakibaniwa katika media kuchezwa kwa ngoma zao kutokana na kutokuwa na majina au kusema kuwa hawana vipaji vya kuimba.

Diamond Platinumza anaamini kuwa Media zake zimekuwa zikitatua changamoto za ajira kwa baadhi ya vijana katika jamii baada ya kumaliza chuo.

Wasafi Tv haijaanza kurusha matangazo ya moja kwa moja lakini tangu uwepo wke imekuwa ikiwapa nafasi wasanii wengi kuonekana kwa nyimbo zao katika Tv hiyo na kuwafanya kujulikana na kutengeneza mashabiki pia.

LEAVE A REPLY