Wasafi Festival kufanya kesho mkoani Iringa

0
106

Tamasha la Wasafi Festival linafanyika leo katika viwanja wa Samora mkoani Iringa baada ya kuzinduliwa ramsi katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

Tamasha hilo itafanyika Iringa kwenye Uwanja wa Samora ambapo wasanii wengine wapya kama Linah, Belle 9 na Afande Sele wameongezeka kwa ajili ya kunogesha burudani hiyo.

Wasanii watakaokinukisha Iringa ukiachilia waliotajwa hapo juu ni One Incredible, Stereo na Nikki Mbishi hawa kwa upande wa Hip Hop, wengine ni Khadija Kopa, Chin Bees, Moko, Young Killer, Dudu Baya.

Baada ya kufanyika mkoani Iringa tamasha hilo litafanyika mkoani Morogoro siku ya Jumapili ya Desemba 2, mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri.

Watakaongezeka kwa Morogoro ni Linah, Afande Sele, Belle 9 na Navy Kenzo ambao watatoa burudani ya kufa mtu katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

LEAVE A REPLY