Warithi wa Prince kupimwa vinasaba

0
120

Jaji Kevin Eide kwenye mahakama ya jimbo la Minesota nchini Marekani amekataa hoja za watu 29 wakiwemo wanaume watano waliodai kuwa nao ni warithi wa marehemu Prince.

Mwanamuziki Prince ambaye alifariki mwezi Aprili kutokana na kuzidisha kwa bahati mbaya matumizi ya dawa za kupunguza maumivu za fentanyl hakubahatika kuacha wosia na hakuwahi kutangaza kuwa na watoto.

Prince ana mali isiyohamishika inayokadiriwa kuwa na thamani ya $300m (TZS 750bn).

Hakimu wa mahakama hiyo ameamuru uchunguzi wa vinasaba ufanyike kwa watu sita wanaodai kuwa na undugu na mwanamuziki huyo.

Watu hao, wanne wanadai kuwa ndugu wa damu au ndugu wa kuchangia wazazi na watu wawili mabinamu.

Uchunguzi huo wa vinasaba tayari umemuondoa mfungwa mmoja kwenye orodha ya warithi ambaye alidai kuwa yeye ni mtoto wa Prince.

LEAVE A REPLY