Wapinzani waonya kumuita Jammeh ‘Kiongozi muasi’ asipong’atuka Jan. 19

0
160

Msemaji wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Gambia, Halifa Sallah amemtahadharisha rais Yahya Jammeh kuwa endapo hatoondoka madarakni baada ya tarehe 19 basi atachukuliwa kama muasi.

Halifa amesema kuwa kuanzia Januari 19, rais Jammeh atakuwa raia wa kawaida na hatokuwa na mamlaka ya kikatiba ya kuviamrisha vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

‘Rais yeyote ambaye muda wake wa kuwa madarakani umemalizika ambaye anachukua silaha dhidi ya rais anayeingia madarakani ambaye muda wake unapaswa kuanza kwa mujibuj wa sheria atachukuliwa na jumuiya ya kimataifa kama kiongozi muasi’

Wakati msemaji huyo akitanabaisha hayo, mshindi wa uchaguzi mkuu kutoka upinzani, Adamma Barrow amesema kuwa anajipanga kwaajili ya kuapishwa mnamo tarehe 19.

LEAVE A REPLY