Wanyama ashinda tuzo ya goli bora la mwezi february

0
211

Mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya na klabu ya Tottenham Hotspurs, Victor Wanyama, amefanikiwa kushinda tuzo ya goli bora la mwezi February katika ligi kuu ya Uingereza.

Wanyama ameshinda tuzo hiyo kupitia goli lake alilowafunga Liverpool katika sare waliyotoka ya kufungana mabao 2-2.

Wachezaji wengine ambao walikuwa wanawania tuzo hiyo ni Danilo na Sergio Aguero (wote kutoka Manchester City) , Mario Lemina (Southampton), Jose Izquierdo (Brighton), Mohamed Salah (Liverpool) na Adam Smith (Bournemouth).

Wakati huo huo kocha Chris Hughton wa Brighton, amefanikiwa kushinda tuzo ya kocha bora ya mwezi huo.

Chris ameisaidia Brighton kushinda alama saba kati ya michezo mitatu ambayo timu yake imecheza katika mwezi wa pili na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya 10 katika ligi kuu mpaka sasa.

LEAVE A REPLY