Wanaume waliotelekeza watoto kuanza kupelekewa barua za wito kesho

0
137

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa kuanzia kesho wanaume wote ambao tayari wametajwa kutelekeza watoto wataanza kupelekewa barua za wito.

RC Makonda amesema kuwa hakutakuwa na kigogo yoyote atakayehitaji kuonana naye kwa siri kama ambavyo wengi wamekuwa wakiomba kufanya hivyo na kueleza kuwa nafasi hiyo haipo.

Amesema kuwa vigogo 107 tayari wametajwa kutelekeza watoto na amewaomba mara wapatapo wito wa barua yake wafike ofisini kwake mara moja kwani watakaokaidi watachukuliwa hatua kali za kesheria.

Wanawake hao walianza kujitokeza siku ya jumatatu katika ofisi ya mkuu wa mkoa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupata msaada wa kisheria baada ya kutelekezewa watoto na wanaume waliozaa nao.

Mbali na zoezi hilo Makonda amesema kuwa wadau mbalimbali wamejitokeza kusaidia kuwalipia watoto hao Bima za afya ili waweze kumudu gharama za matibabu kwa kipindi cha mwaka mmoja.

 

 

 

 

 

 

LEAVE A REPLY