Wanajeshi wa Israel wamuua mtoto wa miaka 12

0
163

Wanajeshi wa Israeli wamemuua kwa risasi ya mpira mtoto wa miaka 12, Mohiyeh al-Tabakhi raia wa Palestina wakati wa maandamano karibu na mji wa Jerusalem.

Wizara ya afya ya mamlaka ya Palestina imethibitisha kutokea kwa mauaji hayo yaliyotokea kwenye eneo la Al-Ram karibu kabisa na Jerusalem.

Mtoto, Mohiyeh alipigwa na risasi kifuani na wanajeshi wavamizi ambayo ilimsababishia shinikizo la damu lililopelekea mauti yake.

Polisi wa Israeli wamedai kutumia mabomu ya machozi wakati wa kuwatawanya waandamanaji hao wa Palestina.

Vurugu kwenye eneo la wapalestina ziliibuka upya mwezi Oktoba mwaka jana na hadi sasa zimeshaua wapalestina 217, waisraeli 34, wamarekani wawili, raia wa Eritrea na raia wa Sudan.

LEAVE A REPLY