Wanafunzi watano wameuawa kwenye maandamano nchini Guinea

0
168

Wanafunzi watano wameuawa na wenginge 30 wamejeruhiwa nchini Guinea wakati vikosi vya usalama vilipopambana nao walipokuwa wanaandamana wakitaka mgomo wa walimu kumalizika.

Wanafunzi walijitokeza kwa wingi na kwa hasira wakaanza kuwatupia polisi mawe kwenye maandamano hayo nchini Guinea.

Maafisa walithibitisha vifo hivyo na kuwalaumu waandalizi wa maandamano kwa kupanga kile kilichotajwa kuwa maandamano haramu.

Mfanyakazi mmoja wa hospitali amesema kuwa waliouawa walipigwa risasi kwa karibu na polisi wa kuzima maandamano.

Waalimu nchini Guina wamekuwa kwenye mgomo wakilalamikia mishahara duni.

LEAVE A REPLY