Wanafunzi wa Kiislam waruhusiwa kuvaa hijab shuleni

0
538

Mahakama ya rufaa ya mji mkuu wa Nigeria, Lagos imetengua hukumu ya awali ya mahakama ya mji wa Suno iliyowazuia wanafunzi wa kike wa kiislam wanaosoma shule za serikali kwenye jiji la Lagos kuvaa hijab wanapokuwa shule.

Hukumu hiyo imepokewa kwa shangwe kubwa na taasisi ya haki za waislam (MRC) lililodai kuwa hukumu hiyo ni ushindi mkubwa kwa utawala wa sheria.

Wasichana wawili wa kiislam walipeleka lalamiko lao kwenye mahakama ya rufaa kupinga uamuzi wa mahakama kuu wa mwaka 2013 uliozuia uvaaji wa hijabu mashuleni.

Majaji watano (waislam wawili kati yao) walioamua kesi hiyo wamedai kuwa zuio la awali linakiuka haki ya kiimani ya wasichana wa kiislam hivyo wametengua hukumu hiyo.

Wasichana wa kiislam walizuiwa kuvaa hijabu kwasababu sio sehemu ya sare za shule.

Bado haijafahamika iwapo upande wa serikali uliofungua kesi hiyo utakata rufaa kwenye mahakama kuu au utaridhika na uamuzi wa mahakama hiyo.

Kwa kiasi kikubwa raia wa Nigeria wamegawanyika kiimani baina ya waislam na wakristu huku kila kundi likiwa na waumini watiifu kwa imani zao.

Mwezi uliopita ahakama ya juu kwenye mji wa Osun pia ilitengua zuio la wasichana wa kiislam kuvaa hijabu wanapokuwa shuleni hali ambayo ilizua sintofahamu kwenye jamii hiyo ambapo wavulana wa kikristu nao wakasisitiza kuvaa kanzu zao za kidini wanapokuwa shuleni.

LEAVE A REPLY