Wanafunzi 24 wazama ziwani mkoani Geita

0
237

Wanafunzi 24 wa Shule ya Msingi Butwa mkoani Geita wamezama katika kisiwa cha Butwa kilichopo ziwa Victoria walipokuwa wanatoka shuleni.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa wilaya ya Geita, Herman Kapufi kati ya wanafunzi hao 24 waliozama wakiwa ndani ya mtumbwi, 21 wameokolewa jana usiku na watatu bado wanatafutwa.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa  ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni baada ya mtumbwi huo kupinduka katika Ziwa Victoria.

Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa wa Geita ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Geita, Ezekiel Kyunga imeelekea sehemu ya tukio kushiriki zoezi la uokoaji.

LEAVE A REPLY