Wama Sepetu akanusha kufulia

0
126

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa taarifa zinazosambaa kuwa amefulia hazina ukweli hata kidogo kwani maisha yake yanaendelea.

Wema Sepetu amekula shavu baada ya kualikwa kama mgeni rasmi kwenye Usiku wa Zanzibar Sweetheart utakaofanyika Zanzibar Beach Resort hivi karibuni.

Wema amesema tayari ameshalipwa kiasi cha shilingi milioni saba hivyo anamshukuru muandaaji wa tamasha hilo kwa kuona umuhimu wake na kwamba ametambua bado anapendwa.

Kutokana na ukimya wake kwenye Mitandao ya kijamii imekuwa ikisemekana kuwa staa huyo amefulia na umaarufu Wake kuisha baada ya skendo yake iliyomchafua mwaka jana.

LEAVE A REPLY