Waliombeza Wema Sepetu wamuomba dawa dawa nao wapungue

0
263

Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa waliokuwa wanamkejeli kuhusu kupungua kwa mwili wake sasa wanaomba dawa anayotumia ili na wao wapungue wawe kama yeye.

Wema amesema kuwa kuna wakati anakosa amani kutokana na maneno ya watu wakiwemo wasanii wenzake walikuwa wanamrushia vijembe kwa kubadili wake lakini sasa wanamsumbua kutaka dawa zake za kupunguza mwili.

“Miezi kadhaa nyuma nilipokuwa na mwili mnene watu walikuwa wakinibeza sana hata wasanii wenzangu lakini sasa baada ya kukondeana huku wamekubali wembamba wangu kunisumbua kutaka dawa niliyotumia na nikapendeza” Alisema Wema Sepetu.

Wema alisema kuwa hata mashabiki wake katika mtandao wa kijamii walikuwa wanamsumbua kutokana na mwili wake kuwa mwembamba badala yake wanamtaka arudishe mwili wake wa zamani wa unene.

Wema Sepetu amepunguza mwili wake ambapo kwasasa anaonekana kuwa mwembamba tofauti na zamani alipokuwa na mwili mkubwa.

LEAVE A REPLY