Walioghushi vyeti kutupwa jela miaka saba

0
339

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa watumishi walio na vyeki feki wakatwe mshahara wa mwezi huu na kufukuzwa kazi pamoja na kifungo cha miaka saba jela.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa majina ya watumishi wenye vyeti feki wapatao 9732 katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Amesema kuwa wenye majina hayo wenyewe wanajijua na majina hayo yachapishwe kwenye magazeti kwasababu wameiibia Serikali.

Rais Magufuli ametumia nafasi hiyo kutaja jina moja la aliyeghushi vyeti kuwa ni Abdalah Polea ila hakutaja ametokea sekta gani ya Umma.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa watumishi hao waliogushi vyeti ni sawa na majambazi, majizi kama yalivyo majizi mengine.

Majina hayo ya watumishi wenye vyeti yamekabidhiwa kwa rais Magufuli na Waziri wa Utumishi wa Umma, Angela Kairuki.

 

LEAVE A REPLY