Wakongwe wa vita ‘wamemsaliti’ Mugabe?

0
140

Chama cha wanajeshi wastaafu na wakongwe wa vita wa Zimbabwe kimetoa taarifa ya kuacha kumuunga mkono rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe.

Chama hicho ambacho kwa muda mrefu kimekuwa bega kwa bega na rais Mugabe kimemlaumu rais Mugabe kwa kile ilichokidai kuwa rais Mugabe amekuwa na tabia za udikteta, mjivuni na amekuwa akiongoza vibaya.

Bado haijawa wazi iwapo kauli hiyo inaungwa mkono na wanachama wote au ni kauli ya baadhi ya wanachama.

Ikulu ya Zimbabwe na chama cha ZANU-PF bado havijatoa kauli yoyote kuhusiana na taarifa hiyo.

Chama hicho kinaundwa na wakongwe wa vita waliopambana pamoja na rais Mugabe kwenye miaka ya 1970 wakati wa kupigania ukombozi wa nchi hiyo kutoka kwenye mikono ya wakoloni.

Migogoro ya kisiasa imekuwa ikilikumba taifa la Zimbabwe mara kwa mara huku lawama kubwa akitupiwa rais Mugabe ambaye hata hivyo ameshatangaza nia ya kugombea tena nafasi ya urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2018.

LEAVE A REPLY