Wakimbizi wa Sudani Kusini wafikia milioni moja

0
166
A displaced child holds the tyre he was using as a toy as he navigates across a muddy patch of ground to go fill an empty bottle with water from a truck, at a United Nations compound which has become home to thousands of people displaced by the recent fighting, in the capital Juba, South Sudan, Sunday, Dec. 29, 2013. Some 25,000 people live in two hastily arranged camps for the internally displaced in Juba and nearly 40,000 are in camps elsewhere in the country, two weeks after violence broke out in the capital and a spiralling series of ethnically-based attacks coursed through the nation, killing at least 1,000 people. (AP Photo/Ben Curtis)

Umoja wa Mataifa umesema kuwa idaidi ya wakimbizi wan chi ya Sudani Kusini wanaokimbilia kwenye nchi mbalimbali wamevuka milioni moja.

Ripoti hiyo mpya ya Umoja wa Mataifa imechapishwa na shirika la kuhudumia wakimbizi duniani la Umoja huo, UNHCR.

Idadi kamili inahusisha zaidi ya watu 185,000 waliokimbia mapigano mapya nchini humo yaliyozuka mwanzoni mwa mwezi wa Julai mwaka huu.

Zaidi ya watu milioni 1.6 wamekosa makazi ndani ya nchi hiyo huku ukosefu mkubwa wa chakula na maji ukitishia uhai wao.

Makadirio ya idadi ya watu nchini Sudani Kusini ipo kati ya milioni 10 na milioni 12 ingwa idadi rasmi haijulikani.

Kwa taarifa hiyo ya UNHCR inamaanisha kuwa zaidi ya 20% ya raia wan chi hiyo hawana makazi kutokana na mapigano hayo.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalizuka mnamo mwezi Disemba 2013 na kuendelea hadi sasa licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani na kuundwa kwa serikali ya Umoja.

 

LEAVE A REPLY