Wakazi kuwasaidia wasanii wa kike

0
105

Mwanamuziki wa hip pop nchini, Wakazi ameweka wazi mipango yake ya kutaka kuwasaidia wasanii wa kike kufikia ndoto zao.

Wakazi ni miongoni mwa wasanii ambao wametoa shoo kali katika tamasha la Sauti za Busara msimu wa 17 ambalo limemalizika jana katika eneo la kihistoria Ngome Kongwe, Zanzibar.

Wakazi amesema amejikita kufanya kazi na wasanii wakike katika bendi yake kwa kuwa anatazamia kusimamia ndoto zao katika muziki.

“Wasanii wa kike wanapata changamoto nyingi wakiwa katika safari ya kutoka kimuziki nimeamua kuwashika mkono ili kuleta mabadiliko katika tasnia yetu, nina wasanii wa kike tu katika bendi yangu”.

Msanii huyo amesema kuwa ameamua kuwasaidia wasanii wa kike kwasababu wasanii wa kike wamekosa msaada kutoka kwa wadau wa muziki.

LEAVE A REPLY