Wakala: Luke Shaw haondoki Manchester United

0
121
498499109JD00053_Manchester

Wakala wa mlinzi wa Manchester United, Luke amekanusha tetesi za kuhama kwa mlinzi huyo kutoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Jonathan Barnett amesema kuwa habari za Luke Shaw kutokuwa na furaha klabuni hapo kutokana na kusugua benchi ni upumbavu usio na msingi.

Shaw ambaye ameichezea United mara 13 tu tangu kutua kwa Jose Mourinho hajaonekana kwenye kikosi cha United tangu Novemba 30 mwaka jana.

Hata hivyo habari za ndani ya Old Trafford zinadai kuwa staa huyo amewekwa kwenye programu maalum kama iliyomuimarisha Mkhitaryan baada ya Mourinho kutoridhishwa na kiwango cha mlinzi huyo.

‘Ana furaha kwenye klabu hiyo na United wanampenda na wanamfurahia’.

Shaw alijiunga na United mwaka 2014 akitokea Southampton kwa ada ya £27m.

LEAVE A REPLY