Wafanyakazi wa maonyesho ya mavazi wafungwa jela kwa kusambaza ‘ukahaba’

0
256

Watu kumi na mbili kati ya 170 wanaojihusisha na biashara ya mavazi na ubunifu wameripotiwa kuhukumiwa vifungo vya jela baada ya kukutwa na hatia ya kusambaza ukahaba kupitia picha za mitandaoni.

Shirika la habari la Ilna limeripoti kuwa watu hao (wanawake nane na wanaume wanne) wanadaiwa kuhukumiwa vifungo vya kati ya miezi mitano na miaka sita na mahakama ya Shiraz.

Pamoja na vifungo hivyo watu hao wanadaiwa kufungiwa kujishughulisha kwa muda na shughuli za mitindo ya mavazi na ubunifu na kusafiri nje ya Iran kwa kipindi cha miaka miwili baada ya kukamilika kwa adhabu zao za vifungo vya jela.

Hata hivyo wakili wa watu hao, Mahmoud Taravat amedai kuwa wateja wake wamekana mashtaka hayo na wanakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu zao.

Mashtaka ya watu hayo yanahusu kuchapisha mitandaoni picha za wanawake wakiwa vichwa wazi kwenye kadamnasi pamoja na kuchohcea uovu kwa wanaume kupitia picha zinazoonyesha maumbile ya wanawake kupitia maonyesho ya mavazi na mfumo wa maisha ya magharibi.

LEAVE A REPLY