Wafanyakazi wa Manji wapandishwa kizimbani Kisutu

0
209

Wafanyakazi wawili wa kampuni ya Quality Group iliyo chini ya Yusuf Manji wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar kujibu mashtaka matatu likiwemo la kufanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali.

Watuhumiwa hao na wengine 14 wanashtakiwa kwa kuzuia afisa Uhamiaji kufanya kazi yake na kukaidi agizo la ofisi ya Uhamiaji na kujaribu kotoroka kupitia Mpaka wa Horohoro walikokamatiwa.

Watuhumiwa hao ni Meneja Mradi Jose Kiran na mwenzake Katibu Mradi Prakash Bhatt Februari 13  walikutwa jengo la Quality Center wakifanya kazi kamawashauri bila ya kibali cha kukaa nchini.

Wamesomewa mashtaka yao mbele ya  hakimu Sprian Mkeha na kupatiwa dhamana ya ml. 5 kila mmoja.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

LEAVE A REPLY