Wafanyabiashara wadogo wafanya maandamano Kenya

0
216

Mamia ya wafanyabiashara wamefanya maandamano katika barabara za eneo la Eastleigh jijini Nairobi nchini Kenya ili kupinga kuvunjwa kwa vibanda vyao vya kufanyia biashara.

Maafisa wa polisi wameharibu vibanda vilivyojaa kandokando ya barabara ambapo huweka bidhaa zao zote kwa ajili ya mauzo.

Operesheni hiyo ya polisi inafuatia malalamiko kutoka kwa wamiliki wa maduka ambao wamesema kuwa wamekuwa wakizuia watu kuingia katika maduka hayo.

Wamiliki wa maduka pia nao wamefunga maduka yao ikiwa ni mgomo wao wa siku tatu wa kutaka baraza la jiji la Nairobi kuwandoa wafanyabishara hao wa bidhaa ndogo ndogo.

Wafanyabiashara ndogo ndogo hawatakiwa katika maeneo ya Eastleigh jijini Dar es Salaam kutokana wanawazuia wafabishara wenye maduka kutofanya biashara zao kwa hali ya utulivu.

 

LEAVE A REPLY