Waandishi wakumbushwa: Mkutano wa JPCC haujadili mgogoro wa mpaka

0
175

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imetoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) unaotarajiwa kufanyika nchini Malawi mapema mwezi Februari na kukanusha kuwa mkutano huo hautaenda kujadili juu ya mgogoro wa mpaka baina ya nchi hizo.

Kwenye taarifa yake wizara hiyo imedai kuwa imelazimika kutoa ufafanuzi wa dhumuni la mkutano huo kwasababu taarifa zilizochapishwa na vyombo vingi vya habari vya nchini siku ya tarehe 27 vilinukuu vibaya dhumuni la mkutano huo.

Taarifa ya wizara hiyo imedai kuwa mkutano huo una lengo la kutathmini utekelezwaji wa makubaliano ya mkutano wa tatu wa JPCC uliofanyika nchini mwaka 2003 na wala hauna ajenda ya kujadili tatizo la mpaka baina ya Tanzania na Malawi.

Ikifafanua zaidi taarifa hiyo imedai kuwa suala la mgogoro wa mpaka tayari lipo mikononi mwa jopo la usuluhishi linaloundwa na viongozi wastaafu Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.

LEAVE A REPLY