Vita kali leo Old Trafford, nani kuibuka mbabe?

0
143

Manchester United leo itaikaribisha Tottenham kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza itakayofanyika katika uwanja wa Old Trafford.

Timu hizo zote zinaingia uwanjani zikiwa na alama 20 tofauti ikiwa ni magoli ya kushinda na kufungwa ambapo machester United wanamagoli mengi zaidi.

Tambo za makocha

Kwa upande wa Pochettino amesema kuwa anaamini timu yake inaweza kushinda bila Harry Kane kutokana na wachezaji wengi kuwa na kiwango kikibwa kwenye timu hiyo hivyo si kweli watashindwa kucheza vizuri bila Kane.

Kocha huyo ameendelea kusema kuwa ni kweli amejisikia vibaya kumkosa mshambuliaji huyo kwasababu ni miongoni mwa washambuliaji bora sana kwasasa Ulaya na duniani kwa ujumla.

Nae Mourinho amesema kuwa watu wasizungumze Tottenham kumkosa Harry Kane mbona yeye anawachezaji wake muhimu na wanakosa mechi hiyo ya ligi kuu, kwanini wamzungumzie Harry Kane.

Mouringo amesema kuwa leo timu yake lazima ishinde kutokana na kujiandaa vizuri na mabeki wake visiki wamerudi kwenye mechi hiyo kama vile Phill Jones na Elick Baily waliokuwa maejeruhi.

LEAVE A REPLY