Viongozi wa Olimpiki ‘wapigaji’ Kenya wazidi kukamatwa

0
99

Aibu ya mwaka inazidi kuiandama michezo nchini Kenya huku viongozi wa kamati ya mshindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini Rio nchini Brazili ikizidi kuumbuka.

Aibu hiyo imekuja baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa tano wa wizi wa fedha na vifaa vya michezo vilivyolengwa kutumiwa na wachezaji kwenye mashindano hayo.

Ben Ekumbo ambaye ni makamu wa rais kamati ya olimpiki ya nchi hiyo na mkuu wa shirikisho la kuogelea nchini humo anadiawa kukutwa chini ya uvungu wa kitanda wakati wa kukamatwa na polisi wanaofuatilia sakata la upotevu wa fedha na vifaa vya wachezaji wa Kenya vilivyotolewa kwaajili ya Olimpiki ya Rio.

Pamoja na kudaiwa kumkuta mewenyewe akiwa chini ya kitanda lakini pia polisi walikuta maboksi ya viatu vya kumbilia vya Nike vilivyolengwa kutumiwa na wanariadha wa nchi hiyo.

Viongozi hao wa kamati ya olimpiki wanatuhumiwa kuiba fedha taslimu na vifaa vyenye thamani ya zaidi ya £6.4m ambavyo kwa pamoja vilipaswa kutumiwa na wachezaji.

LEAVE A REPLY