Video vixen Bongo adai kuendelea kupiga picha za utupu mitandaoni

0
3544

Video vixen Bongo, Sasha  Kassim ameibuka na kusema kuwa  ataendelea kuweka picha zake za utupu mitandaoni.

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza alitangaza vita na wasichana wote ambao wanaanika picha zao za utupu mitandaoni na kuahidi kuwafungia kazi zao za sanaa endapo wataanika picha hizo.

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu hatimaye Sasha  Kassim amefunguka kuwa ataendelea  kupiga picha za nusu uchi.

Sasha alisema kuwa anajiandaa kupiga picha nyingine ambazo kama ni nguo za ndani zitaonekana nadhifu na zenye kuvutia na pia zitapungua ‘ukali’.

Amesema kuwa “Nilipotea kwa sababu niliibiwa akaunti yangu ya Instagram, si unajua ilikuwa na picha nyingi sana ila sasa hivi najiandaa kupiga picha nyingine mpya zitakuwa zikinionyesha sehemu zangu za mwili lakini zitakuwa zenye kujistiri kidogo”.

 

 

LEAVE A REPLY