Video mpya ya Ney wa Mitego yazua utata

0
14

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amekiuka kiapo alichomuahidi mama yake baada ya kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la Go Baba ambayo baadhi ya vipande katika video hiyo inaonesha matendo ya kutisha kama vile Nay kunywa kimiminika kinachofanana na damu.

 

Nay aliachia wimbo wake unaoitwa Mungu Yuko Wapi ambao uliibua utata wa kimapokeo ikiwemo ya kupingwa na baadhi ya mashabiki kwa kile kilichotajwa kuwa mashairi yake yalikuwa yakikosoa uwepo wa Mungu.

  

Video hiyo ilileta utata siyo tu kwa mashabiki wake, bali hadi kwa mama yake, Nay. Mama huyo aliibuka na kudai kuwa video hiyo ilimchukiza na kumtaka Nay aifute haraka.

 

Nay hakuifuta licha ya kwamba alikiri kupewa maeleko hayo na mama yake ambapo alimuapia kwamba hatafanya tena video au wimbo wa aina hiyo.

 

Nay amerudia jambo kama hilo baada ya kuachia video ya wimbo wake huo ambayo inafanana kwa kiasi kikubwa na video ya Mungu Yuko Wapi.

 

Baadhi ya vipande katika video hiyo mpya iliyoongozwa na muongozaji Joowzey kutoka Tanzania inaonesha matendo ya kutisha kama vile Nay kunywa kimiminika kinachofanana na damu.

LEAVE A REPLY