Video: Hii ndio sababu Fid Q ni bora kuliko Mr II na Profesa Jay?

0
630

Ni mastaa wangapi wa Bongo ambao wana vipaji zaidi ya kuimba au kuigiza movie? Ni kweli kuwa Mr. II a.k.a Sugu kwa sasa ni mwanasiasa anayeelekea kwenye ukongwe na ni kweli kuwa Profesa Jay naye anafuata nyayo hizo.

Lakini je, ukiacha siasa ni vipaji gani vingine walivyonavyo mastaa hawa?

Ukweli ni kuwa unaweza kuwatafuta wenye vipaji vingine na ukawapata wachache na katika hao wachache utakutana na jina la Fareed Kubanda a.k.a Fid Q.

Staa huyu wa Mwanza a.k.a NGOSHA ana kipaji kikubwa zaidi ya kuandika mashairi na kurap kwa hisia.

Fid Q pia ni muandishi mzuri wa vitabu. Staa huyo anatarajia kuweka historia kwenye tasnia ya muziki hapa Bongo pindi atakapozindua albamu yake ya KITAALOJIA baadae mwaka huu.

Fid Q amedhamiria kuzindua TWO in ONE packages ambapo atazindua albamu hiyo pamoja na kitabu chake ‘THE SWAHILI KID’ ambacho kwa mujibu wa maelezo yake, kitabu hicho kimebeba maelezo ya albamu zake zote 3 zinazotambulika hadi sasa.

Tazama ngoma ROHO aliyomshirikisha Christian Bella.

LEAVE A REPLY