Video: Biff ya AY na marehemu Steven Kanumba hii hapa

0
1408

Ni watu wachache sana walikuwa wanajua kuwa mastaa wa Bongo, AY na Kanumba walikuwa washkaji lakini pia walikuwa mahasimu.

Huenda kutofautiana kwa tasnia wanazofanyia kazi kumepelea mastaa hao kutotambulika kama washkaji lakini ukweli ni kuwa mastaa hao walikuwa marafiki ‘ingawa hawakuwa maswahiba’.

Ila ilifika mahali ambapo AY aliweka urafiki pembeni na kudai haki ya kazi yake; kisa? Moja ya ngoma zake ilisikika kama sound track kwenye movie ya marehemu Kanumba.

Ingawa Kanumba alijaribu kuchukulia ishu hiyo kwa masihara lakini AY aliikomalia na kwenda na mwanasheria hadi ofisini kwa Kanumba ambapo walimalizana kwa AY kulipwa chake siku hiyo hiyo.

Na baada ya hapo, ilipita miaka miwili na zaidi Kanumba akimkaushia AY na AY akimkaushia Kanumba kwasababu ya MKWANJA waliodaiana.

Haikuwa BIFF ya kutajiana mapungufu bali ‘makosa ya kuchukuliana POA kwenye kazi’.

Hebu watu wachukue hii na wajifunze.

Tazama video hiyo kuanzia dakika ya 19:30

LEAVE A REPLY