Victoria Kimani awapa makavu wasanii wa kiume wa Afrika

0
37

Mwanumuziki kutoka nchini Kenya, Victoria Kimani ameatolea uvivu wasanii wa kiume Barani Afrika wanaotembea kifua mbele kuwa wanautangaza muziki wa Afrika Ulimwenguni.

Kauli ya mwanamuziki huyo unakuja baada ya kuwepo kwa wimbi kubwa la wasanii wa kiume wa Afrika wanaosema kuwa wanafanya muziki kwa kuiwakilisha Afrika wakati siyo kweli.

Mwanamuziki huyo ameandika kuwa wasanii hao wanapaswa wafanye kazi kwanza na wasanii wakike waliopo Afrika kabla ya kujitapa kuwa wanaiwakilisha Afrika duniani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Victor Kimani ameandika “Fanyeni kazi na wasanii wakike wa Afrika kabla ya kupiga kelele mnautangaza muziki wa Afrika Ulimwenguni.

Victoria Kimani ni mwanamuziki anayefanya vizuri kwa ukanda wa Afrika Mashariki kwa wasanii wa kike ambaye anataka wasanii wa kiume wa Afrika kufanya nyimbo na wasanii kike wa Afrika.

LEAVE A REPLY