Vee Money: Sina haraka ya kupata mtoto na Jux

0
667

Staa wa Bongo fleva, Vanessa Mdee (Vee Money) amsema kuwa hana haraka ya kupata mtoto na mpenzi wake ambaye pia ni mwanamuziki Jux na kwamba kwasasa watoto wapo wengi wa kuwalea.

Vanessa Mdee amedai kuwa hana haraka ya kupata mtoto na mpenzi wake Jux na kudai kwa sasa wapo watoto wengi wa kulea akiwepo mtoto wa Diamond Platnumz, mtoto wa Shetta.

Mbali na hilo Vanessa Mdee amesema kuwa mara nyingi anajitahidi kufanya media tour katika nchi za watu kutokana na ukweli kwamba watu wa nje ni wazito sana kupokea kazi za wasanii ambao siyo wao.

Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwasasa ndani na nje ya nchi ambapo amefanya kazi tofauti na baadhi ya wasanii wa nje kama K.O kutoka Afrika Kusini na wengine wengi.

Vanessa Mdee kwasasa yupo katika uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki mwenzie Jux ambapo hadi sasa ndiyo Couple inayoonekana kufanya vizuri katika wasanii wa Bongo fleva kwasababu toka mahusiano yao yaanze hawajatofautiana.

LEAVE A REPLY