Vee Money aogopa ndoa

0
78

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka na kuweka wazi kuwa anaogopa sana kufunga ndoa licha ya kwamba umri wake alionao unamruhusu kufanya hivyo.

Vee Money amesema licha ya kwamba ana umri wa miaka 30 kwa sasa, lakini hajawaza kuolewa kwa sababu anaogopa atabanwa na majukumu ya ndoa na kushindwa kufikia malengo aliyonayo kwasasa ila hapo baadae atafanya hivyo.

Vanessa amesema kuwa umri wangu umefikia wa kuingia kwenye ndoa, lakini hawezi kwani ana malengo makubwa ambayo bado ajayatimiza hadi sasa hivyo.

Mwanamuziki huyo ameongeza kwa kusema kuwa anahofia akiingia kwenye ndoa kuwa atabanwa na kushindwa kutimiza malengo hivyo hawezi kukurupuka.

Vanessa amekuwa kwenye uhusiano wa miaka mingi na Mpenzi wake ambaye pia ni Msanii wa Bongo fleva Juma Jux.

LEAVE A REPLY