Vanessa Mdee azindua bidhaa zake za viatu

0
62

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amezindua bidhaa zake za viatu maalum kwa wanafunzi hasa wasichana alizozipa jina la ‘Bora Star by Vanessa Mdee’.

Kupitia ukurasa wake wa twitter alituma ujumbe na picha akionyesha viatu hivyo huku akisema imekuwa ni ndoto yake kwa muda mrefu

Ilikuwa ndoto yangu kutengeneza bidhaa itakayonufaisha na kuboresha maisha ya msichanawa kitanzania ama kiafrika na leo nimetimiza ndoto yangu, nasema asante Mungu,” ameandika Vanessa.

Vanessa Mdee anaingia kwenye orodha ya wasanii ambao waliongiza bidhaa zao sokoni akiwepo Alikiba ambaye ameingiza bidhaa za Mofaya pamoja na Mwana FA ambaye ameingiza bidhaa za manukato.

LEAVE A REPLY