Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amevalishwa pete ya uchumba na mpenzi wake Rotimi ambaye ni msanii wa filamu ambapo wote kwa sasa wanaishi nchini Marekani.
Â
Videos ambazo zimepostiwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha Rotimi akiwa amepiga magoti mbele ya Vanessa huku akimvalisha pete hiyo ya uchumba, kisha wakakumbatiana na kuanza kupigana mabusu.
Â
Mwanzoni mwa mwezi wa kumi mwaka 2020, Vanessa na Rotimi walishea picha mitandaoni zikiwaonyesha wamechorana tattoo zenye majina yao kwenye miili yao.
Â
Penzi la wawili hao lilianza Oktoba 2019, baada ya Vanessa kuachana na mkali wa RnB Bongo, Juma Jux, ambapo walidumu kwa miaka sita.